Jukumu la baraza la waamuzi ni nini, na nani anaweza itwa kuhudumu katika baraza la waaamuzi?

Mwanasheria azungumza mbele ya baraza la waamuzi mahakamani

Mwanasheria azungumza mbele ya baraza la waamuzi mahakamani Source: Getty Images/RichLegg

Kila raia wa Australia ambaye amesajiliwa kupiga kura, anaweza itwa kutoa huduma katika baraza la waamuzi mahakamani.


Ila, nini kinahusika uki itwa kuwa mmoja wa waamuzi mahakamani? Na jukumu la waamuzi hao ni nini?

Baraza la waamuzi ni sehemu mhimu ya mfumo wa sheria wa Australia. Ni wajibu wa raia wa Australia kuhudumu katika baraza la waamuzi, unapo itwa kufanya hivyo na, watu wanaweza tozwa faini wasipofanya hivyo.

Huduma ya baraza la waamuzi, huruhusu wanachama wa jamii, kushiriki katika utoaji wa haki.


Share