Mageuzi hayo yata wasilisha kile ambacho serikali ina ita “kifungo cha watu wazima kwa uhalifu wa watu wazima”, na yata ondoa msisitizo kwa kutumia kizuizi kama suluhu ya mwisho.
Kikao cha umma, kilicho jadili muswada huo kilifanywa katika eneo la Kaskazini Queensland Jumanne 3 Disemba, kusikiza mawasilisho ya waathiriwa wa uhalifu.
Wakaaji wa Kaskazini Queensland ambao wame pitia uzoefu wa uhalifu wa vijana, walipewa fursa yaku changia uzoefu wao.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa, lilisema uamuzi huo una kiuka sheria ya kimataifa na ni “upuuzaji mubaya wa haki za watoto."
Licha ya ukosoaji huo Mwanasheria Mkuu wa jimbo hilo Deb Frecklington amesema serikali ya jimbo ita endelea mbele na muswada huo, hatua ambayo itakuwa nikupita juu ya sheria ya haki za binadam ya Queensland.
Wakati huo kamati ya Haki, Uadilifu na usalama wa jamii, inatarajia kuwasilisha ripoti yake Ijumaa 6 Disemba, kabla muswada huo uharakishwe kuwasilishwa nakujadiliwa ndani ya bunge la jimbo hilo wiki ijayo.