KISWA: "Wanafunzi wakimataifa wapewe msamaha wakutolipa karo"

Bi Tabitha, Mwenyekiti wa KISWA

Bi Tabitha, Mwenyekiti wa KISWA Source: SBS Swahili

Janga la COVID-19 limewaathiri sana wanafunzi wakimataifa kote nchini Australia, janga hilo limesababisha changamoto nyingi pia kwa familia za wanafunzi hao katika nchi zao za asili.


Wengi wao wamepoteza ajira zao, hali ambayo ime waweka hatarini kukosa hela zakutosha kulipa karo katika taasisi wanako somea.

Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, mwenyekiti wa shirika la Kenyans in Sydney Welfare Association (KISWA) Bi Tabitha, aliweka wazi hatua ambazo shirika lake limechukua, kuwasaidia wanafunzi ambao wame athiriwa na janga hili la COVID-19.


Share