Kuelewa jinsi maduka ya dawa yanavyo fanya kazi Australia

Male pharmactist portrait

Male pharmactist portrait Source: AAP

Nchini Australia, wafamasia hutoa dawa zilizo agizwa nama daktari pamoja na ushauri wa huduma ya afya, kuelimisha jumuiya kuhusu matumizi salama ya dawa na kuzuia ugonjwa.


Kama una umwa na daktari wako ana kuagizia dawa, hatua inayo fuata ni kutembelea duka la dawa iliyo karibu ya unako ishi kuchukua dawa.

Katika makala haya ya Australia ya fafanuliwa, tuna tazama jinsi mfumo wa duka ya dawa Australia hutumika, ili ujue chaku tarajia unapo tembelea duka la dawa.

Wa famasia ni miongoni mwa wataalama wa huduma ya afya wanao patikana kwa urahisi nchini Australia, wao hutoa aina mbali mbali za huduma.

Duka za dawa huwa na aina mbali mbali za madawa na bidhaa za huduma ya afya. Duka za dawa za jumuiya, huwa hudumia wagonjwa katika sehemu zinapatikana, wakati duka za dawa ndani ya hospitali, huwa hudumia wagonjwa ambao wako ndani ya hospitali.

Nchini Australia, dawa nyingi za kawaida iwapo ni kwa magonjwa ambayo haya tarajiwi au hali ya afya ya muda mrefu, ina hitaji agizo la dawa kutoka kwa daktari wako. Agizo hizo za dawa hujazwa katika duka la dawa.

Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia yafafanuliwa kwa taarifa muhimu na, vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Je una swali lolote kuhusu au pendekezo ya mada? tutumie barua pepe kwa [email protected]

Share