Mahakama yasema mtihani wa tabia unao tumiwa kuondoa maelfu ya watu chini Australia, haustahili tumiwa kwa wakimbizi

Wanaharakati wa wakimbizi waandamana nje ya kizuizi ya uhamiaji cha Villawood

Wanaharakati wa wakimbizi waandamana nje ya kizuizi ya uhamiaji cha Villawood Source: AAP

Wakimbizi ambao wamenyimwa viza au viza yao imefutwa kwa misingi ya tabia, kwa sasa wanaweza hoji uamuzi wa serikali.


Kwa upande wa hukumu hiyo, Bi Battison ame andikia idara ya maswala ya nyumbani akiomba tathmini ifanyiwe kwa wateja wengine 14, ambao wako kizuizini walio nyimwa viza kwa misingi ya tabia.

Mnamo mwezi Agosti mwakajana, waziri wa uhamiaji David Coleman alisema kuwa sera tata za serikali zilisaidia kufuta viza 4,700 za wahalifu wakigeni katika miaka sita iliyo pita, idadi ambayo ni mara saba zaidi ya idadi ambayo chama cha Labor kiliondoa katika miaka sita ya nyuma.

Serakali bado inaweza kata rufaa kwa uamuzi huo, mbele ya mahakimu wote wa mahakama ya shirikisho au mahakama kuu.

 


Share