Mahakama yazima ndoto ya Edgar Lungu

Rais mstaafu wa Zambia Edgar Chagwa Lungu.jpg

Mahakama ya katiba ya Zambia imesikiza ombi la Rais mstaafu wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu lakupewa ruhusa yakuwania urais wa taifa hilo.


Licha yaku ingia mahakamani akiwa na matumaini yakupata hukumu nzuri kwa kesi yake, Bw Lungu na wafuasi wake wame elezea masikitiko yao kwa uamuzi wa mahakama hiyo kumzuia kuwania wadhifa wake wa zamani.

Katika hukumu yake mahakama ilisema Bw Lungu hastahiki kuwania urais wa Zambia kwa sababu ame hudumu tayari kwa mihula miwili. Mhula wakwanza ukihesabiwa kuanza 2015-2016 baada ya Bw Lungu kurithi wadhifa huo kutoka hayati Michael Sata aliye aga dunia akiwa madarakani.

Mahakama imesema muhula wa pili wa Bw Lungu uli anza Septemba 2016 hadi Agosti 2021.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share