Hii ni baada ya mpango huo kukataliwa na kubainisha migawanyiko mikubwa ndani ya chama chake.
Sunak anakabiliwa na changamoto kubwa sana katika kipindi chake cha mwaka mmoja madarakani wakati akijaribu kuwazuia wabunge wa chama hicho wa mrengo wa kulia wasipinge matakwa yao ya kuitaka Uingereza kuachana na mikataba ya kimataifa na kuwa na sera yake yenyewe ya uhamiaji.
Waziri wake wa uhamiaji alijiuzulu siku ya Jumatano na Sunak anakabiliwa na maswali kama anaweza kufanikisha sera yake kuu kupitia kura itakayopigwa katika bunge.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa hiyo pamoja na zingine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.