Anthony Albanese azindua jeki ya kihistoria ya thamani ya $8.5 bilioni ya matibabu bila malipo

ANTHONY ALBANESE ANNOUNCEMENT LAUNCESTON

Australian Prime Minister Anthony Albanese speaks during a policy launch event in Launceston, Tasmania, Sunday, February 23, 2025. (AAP Image/Rob Burnett) NO ARCHIVING Source: AAP / Rob Burnett/AAPIMAGE

Waziri Mkuu Anthony Albanese, Jumapili mchana alizindua ahadi yaki historia kwa Medicare, kama lengo la kampeni ya uchaguzi mkuu wa shirikisho wa 2025 wa chama cha Labor.


Serikali imetangaza jeki ya thamani ya dola bilioni 8.5, kwa muda wa miaka minne, huo ni uwekezaji mkubwa zaidi katika miaka 40, wakupanua utoaji wa huduma zaki matibabu bila malipo pamoja naku punguza gharama zama GP.

Upinzani wa mseto nao hauku chelewa kutoa ahadi sawia ya uwekezaji kama huo kwa Medicare, wakidai kuwa chama cha Labor kime dhoufisha mfumo wa afya wa umma wa Australia.

Serikali ya Labor ina lengo laku hakikisha huduma tisa kati ya kumi kwama GP, zitakuwa bure kufikia mwisho wa muongo kwa kuongeza maratatu motisha ya huduma ya matibabu bila malipo, kwa kuongeza huduma milioni 18 kila mwaka na kuokolea familia milioni 859 kufikia mwaka wa 2030.

Mpango huo unajumuisha- udhamini wa wauguzi 400 pamoja na mradi mkubwa zaidi nchini Australia wa mafunzo yama GP kwa madaktari 2,000.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share