Mfungo wakidini ni nini, na unaathiri vipi afya?

Familia yajiaandaa kufanya futari ya Ramadan

Familia yajiaandaa kufanya futari ya Ramadan Source: Getty Images/mustafagull

Unapo ishi katika nchi yenye tamaduni nyingi kama Australia, kuna uwezekano utakutana au kuwa na marafiki kutoka tamaduni au dini mbali mbali.


Ni mhimu kuweza kuelewa sifa zakidini na kitamaduni za jamii zenye tamaduni na lugha tofauti, hali ambayo husaidia mshikamano zaidi katika jamii.

Moja ya mazoea haya ni mfungo wakidini, ambao hufanywa na dini nyingi tofauti. Katika makala haya, tuta chunguza jinsi mfungo wakidini unavyo athiri afya ya mwili, nakama kunaweza kuwa manufaa yoyote.

Wataalam wa afya husisitiza umuhimu wakuwa na usawa wa chakula, na wanapendekeza kuzungumza na GP, au mtaalam wa lishe kabla yakuanza mfumo mpya wa lishe.


Share