Jamii toka tamaduni tofauti, za kasirishwa kwa mageuzi ya mafao ya wahamiaji

Wanajamii toka tamaduni tofauti wachangia vyakula

Wanajamii toka tamaduni tofauti wachangia vyakula Source: Western Sydney Migrant Resource Centre

Wanajamii toka tamaduni tofauti wame sema wame shangazwa kwa sheria mpya ambazo, zitawalazimisha wahamiaji wengi kusubiri muda wa miaka minne kabla wafuzu kupewa malipo ya ustawi.


Upinzani wa shirikisho umepokea ukosoaji mkali kwaku unga mkono sheria hiyo, inayo ongeza muda ambao wahamiaji wanastahili subiri wanapo wasili nchini kupokea mafao ya ustawi.

Sheria hiyo ilipitishwa ndani ya bunge la shirikisho usiku wa Jumatatu 3Disemba2018.


Share