Moja ya madhara ya hatua zakudhibiti maambukizi ya virusi vya UVIKO-19, ambazo serikali na mamlaka husika ziliweka ni kwamba matukio kama hayo ya Africultures Festival yali ahirishwa kwa zaidi ya miaka mbili kote jimboni New South Wales.
Ila, baada ya mamlaka kuondoa vizuizi hivyo, waandalizi wa tamasha hiyo walituma mwaliko kwa jamii ihudhurie tamasha hiyo tena. Na kama ilivyo kawaida katika tamasha hiyo, wamiliki wa bidhaa mbali mbali hukodi vibanda nakuandika bidhaa zao katika mabanda waliyo kodi kwa ili wateja na watakao hudhuria tamasha hiyo wapate fursa yaku tazama bidhaa hizo na hata kununua vinavyo wavutia.
SBS Swahili ilitembelea kibanda cha Afro Jewelery, ambako mmiliki wa kibanda hicho Bw Mwenda alifunguka kuhusu bidhaa alizo kuwa aki uza pamoja na utaratibu waku agiza bidhaa hizo kutoka Kenya hadi zinapo wasili Australia.