Mwongozo wa makazi: Jinsi yakujiandaa na usahili kwa ajili ya kazi

Jopo lafanya usahili wa kazi ndani ya ofisi

Jopo lafanya usahili wa kazi ndani ya ofisi Source: Getty Images

Kupata ajira kwa mara ya kwanza au kutafuta kazi mpya, kunaweza kuchukua muda mrefu nchini Australia.


Kwa hivyo wakati mwishowe unaitwa kwa ajili ya mahojiano au usahili wa kazi, ni taarifa ya kufurahisha mwanzoni, lakini pia inaweza kuwa usumbufu mkubwa.

Njia pekee ya kufanya vizuri wakati wa usahili ni kuwa tayari na kuwa na wazo la nini cha kutarajia. Natumaini utapewa nafasi hiyo, lakini usikate tamaa ikiwa haitafanyika hivyo. Ni kawaida kulazimika kupitia usahili kadhaa kabla ya kupata kazi.

Hakikisha tu unajifunza kutoka kwa kila usahili, kile umefanya vizuri na kile unachoweza kuboresha. Kwa njia hiyo, utaenda kwenye usahili ujayo ukiwa umejiandaa vizuri.


Share