Matangazo hayo ambayo yanasema waziri mkuu mwenyewe atafaidi kupitia makato ya ushuru wamakampuni, yana peperushwa katika maeneo bunge ambako chaguzi ndogo zitafanywa.
Wakati huo huo, matokeo ya kura mpya ya maoni yame onesha wapiga kura wengi wana endelea kumupendelea Bw Turnbull kuliko Bw Shorten kama waziri mkuu.
Matokeo ya kura ya maoni ya Fairfax/Ipsos yame mpa Bw Turnbull 51% ya kura dhidi ya Bw Shorten ambaye alipokea 33% ya kura hiyo.
Hata hivyo serikali ya mseto ina endelea kuvuta mkia nyuma ya chama cha Labor, katika kura ya upendeleo ya vyama viwili.
Kura hiyo ime baini kuwa 47% ya wapiga kura walio husika katika zoezi hilo, wanaunga mkono serikali ya mseto ilhali, 53% ya wapiga kura wanapendelea chama cha Labor kuongoza taifa.
Kura hiyo ya maoni ilifanywa punde baada ya makato ya ushuru wa mapato binafsi wa serikali, yenye thamani ya dola bilioni 144, kupitishwa ndani ya bunge la taifa wiki jana.