Katika wilaya ya Australian Capital Territory wanafunzi watarejea shuleni Jumatatu 3 Februari, na katika jimbo la Magharibi Australia wanafunzi watarejea shuleni tarehe 5 Februari.
Nao wanafunzi katika majimbo ya Tasmania na New South Wales watarejea shuleni Alhamisi 6 Februari.
Wakati huo huo janga la gharama ya maisha lina endelea kuweka shinikizo kwa familia zinazo lipa karo ya shule.
Sasa, utafiti mpya umefichua ambako baadhi ya sehemu ghali zakusomea nchini Australia zilipo na ambako familia zinaweza mudu.