Rais Tshisekedi awarai vijana wajiunge na jeshi kupambana na M23

African Union President and President of Congo Democratic Republic Felix Tshisekedi

African Union President and President of Congo Democratic Republic Felix Tshisekedi Credit: EPA/LUDOVIC MARIN / POOL MAXPPP OUT/AAP Image

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, amewarai vijana kujiunga kwa wingi na jeshi la taifa kusaidia kupambana na waasi wa M23 wanaojaribu kukamata maeneo makubwa zaidi mashariki mwa nchi hiyo.


Katika hotuba hotuba kwa taifa iliyorushwa kwa njia ya televisheni, Tshisekedi amewahimiza vijana kuingia jeshini akisema wao ndiyo wanabeba dhima ya ulinzi wa Kongo.

Hata hivyo, kundi la waasi wa M23 limesonga mbele kwenye uwanja mwingine wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa kuteka wilaya mbili katika jimbo la Kivu Kusini, vyanzo vya eneo hilo vimeiambia AFP Jumatano.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share