Taarifa ya habari 01 Septemba 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Utafiti mpya unaonyesha Waaustralia wengi watapata chanjo ya COVID-19 ikiwa moja itapatikana, Bajeti ya New South Wales iliyoahirishwa imepangwa kutolewa tarehe 17 Novemba na Jamii zinazoishi karibu na mpaka wa New South Wales na Victoria zitafurahia vikwazo vya kusafiri kulegezwa kuanzia Ijumaa tarehe [4 Septemba].


Msomi wa uhusiano wa Wachina anasema kitendo cha kushikiliwa kwa mwandishi wa habari wa Australia nchini China kinatuma ujumbe mbaya kwa wafanyakazi wengine nje ya nchi ambao wana maoni hata kama hawasemi.

Mtangazaji wa Televisheni Cheng Lei amekuwa kizuizini tangu Agosti 14 na wafanyakazi wa kibalozi wa Australia wanamsaidia lakini haijulikani ni kwanini anazuiliwa nje ya nchi.

Mawakili wanapigania kuhakikisha wafungwa wa pwani ya Nauru na huko Papua New Guinea wanaweza kuomba haraka kupata huduma ya haraka kama sehemu ya rufaa ya Mahakama Kuu leo [1 SEP 10AM]


Share