Kamati ya Seneti, yaonywa dhidi yakubinafsisha mfumo wa utoaji wa viza za Australia

Malisa Golightly azungumza katika kikao cha kamati ya Seneti ya sheria na maswala yakikatiba

Malisa Golightly azungumza katika kikao cha kamati ya Seneti ya sheria na maswala yakikatiba Source: SBS

Wataalam wa uhamiaji wameonya kuwa mpango wa usindikaji wa viza nje ya mifumo ya sasa, wenye thamani yamabilioni ya dola, unatishia uadilifu wa mfumo wa uhamiaji wa Australia.


Idara ya maswala ya ndani imesisitiza kuwa hakuna ajira zitakazo potezwa ila, wakosoaji wa mpango huo wamedai kuwa, hatua hiyo haifanyi chochote kushughulikia maombi ambayo yame wasilishwa tayari.

Licha ya malalamishi hayo yote, serikali ya shirikisho inataka mfumo huo utakao ongozwa na kampuni binafsi, kuwa mtandaoni kufikia mwaka ujao.


Share