Kwa sasa itawabidi raia watarajiwa, wajifunze kuhusu uhuru wakusema nakujieleza, umuhimu wa demokrasia, pamoja na usawa wa fursa.
Mohammad Al-Khafaji ndiye mkurugenzi mkuu wa shirika linalo wakilisha jamii zenye tamaduni tofauti nchini Australia, linajulikana kwa ufupi kama ((FECCA)). Amesema kuwa kuna takriban maombi 150,000 ambayo yame wasilishwa ya uraia, na muda wastan wakusubiri jibu ni takriban miaka mbili.
Ameongezea kuwa hali hiyo haikubaliki na muda huo wakusubiri unastahili punguzwa, kwa ajili yakuwapa wa Australia watarajiwa uhakika. Mtihani huo mpya, uta anza tumiwa kuanzia katikati ya Novemba 2020.