Waustralia pia wanahamisha fedha zaidi nje ya nchi kuliko hapo awali, lakini gharama za siri zinaweza kuwa kubwa sana. Wakala mbalimbali wa utumaji pesa wana kikomo cha kiwango tofauti cha kiasi cha fedha ambazo huwaruhusu wateja kutuma nje ya nchi.
Hata hivyo, chini ya sheria ya Shirikisho la sasa, taasisi zote za fedha za Australia zinahitajika kutoa taarifa za fedha kwa kiwango cha $10,000 au zaidi kwa mdhibiti AUSTRAC, ikiwa ni pamoja na maelezo ya wamiliki wa akaunti husika.
Taarifa za Akaunti za Australia na Kituo cha Uchumbuzi husimamia shughuli za kifedha ili kutambua matukio ya ubatilishaji fedha chafu, uhalifu uliopangwa na ukwepaji wa kodi.