Mwongozo wa Makazi: Je! Unapaswa jenga au nunua nyumba yako?

Familia yapumzika ndani ya nyumba

Familia yapumzika ndani ya nyumba Source: Getty Images

Wakati umiliki wa nyumbani umepungua katika miaka ya hivi karibuni, bado inachukuliwa kuwa sehemu muhimu ya maisha ya Waustralia.


Ikiwa utanunua nyumba iliyokwishajengwa au kujenga mpya, wataalamu wa masuala ya nyumba wanasema, chaguo zote mbili zina faida zake.

Unapoanza kutafakari kuhusu kumiliki nyumba, jiulize maswali kadhaa: Umepanga muda gani wa kukaa huko? Wapi unataka kuishi? Unataka nyumba ya aina gani? Nini unaweza kumudu? Je! Unataka kuboresha kwenda kwenye nyumba nzuri baadaye?

Mara baada ya kujibu maswali haya, inapaswa kukusaidia kuamua chaguo bora kwako.


Share