Kufikia mwaka wa 2020, nyumba nyingi na sehemu za biashara, zitakuwa zimeunganishwa na huduma hii.
Frank Mtao anatuangazia juu ya nini tunahitaji kujua na mpango upi wa huduma ni mzuri kabla ya kubadili na kuhamia mtandao huo wa NBN.
Kwa maelezo ya ziada kuhusu jinsi mtandao wa NBN unavyotolewa na wakati ambao utafika eneo unaloishi, tembelea tovuti hii: nbnco.com.au.
Kama una swali kuhusu mpango wa simu au internet, wasiliana na shirika unalotumia huduma zao za simu na internet au tafuta shirika tofauti.