Mwongozo wa Makazi: Haki ya usalama kazini

Vifaa vya usalama kazini

Vifaa vya usalama kazini Source: pixabay public domain


Kwa mujibu wa sheria, waajiri wana wajibu waku unda mazingira salama, kwa ajili yakupunguza majeraha na ugonjwa katika sehemu za kazi.

Hata hivyo ofisi ya takwimu ya Australia, ime baini kuwa; kati ya mwaka wa 2013 hadi 2014, idadi ya watu inayo zidi nusu milioni, waliathirika kupitia jeraha au ugonjwa katika sehemu zao za kazi.

Baadhi ya kazi zina hatari kuzidia zingine, hata hivyo wafanya kazi kutoka jumuiya ambazo kiingereza si lugha yao ya kwanza huwa katika athari zaidi.

 

 


Share