Stephen Tongun afunguka kuhusu uigizaji nchini Australia

Stephen Tongun akishiriki kwenye tamasha ya mitindo mjini Adelaide, Australia

Stephen Tongun akishiriki kwenye tamasha ya mitindo mjini Adelaide, Australia Source: SBS Swahili

Stephen Tongun ni mwanasheria, mjasiriamali na mwigizaji katika tasnia ambako waigizaji wenye asili ya Afrika ni nadra.


Bw Tongun ni mwanaharakati pia wa haki za binadam, na alipata fursa yakutumia uzoefu wake katika tamthilia ya Stateless ambayo unaweza tazama kwenye mtandao wa Netflix na ABC IView nchini Australia.

Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS Bw Tongun, aliweka wazi kilicho mshawishi kuwa mwigizaji licha yakuwa yeye ni mwanasheria na mjasiriamali tayari, pamoja na uhaba wa waigizaji weusi na changamoto za uigizaji.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Share