Swahili Taarifa ya Habari 1 Aprili 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Get the SBS Audio app

Other ways to listen


Published 1 April 2025 1:34pm
By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Waziri wa Ajira na mahusiano ya kazini, Murray Watt, ame kosoa ahadi ya upinzani yaku futa baadhi ya mageuzi ya mahusiano ya viwanda ya Serikali ya Labor.


Sherehe za Eid Al-Fitr zina endelea miongoni mwa wa Islamu wa Australia, sherehe hiyo ina ashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan. Katika Msikiti wa Omar ambao uko katika kitongoji cha Auburn magharibi Sydney, zaidi ya watu elfu 20 wali jumuika kwa ibada pamoja na sherehe mtaani.

Soko la nyumba la Australia limerejea katika viwango vya juu vya ongezeko ya bei ya asilimia 0.4, kwa bei za nyumba kitaifa katika mwezi wa Machi. Ripoti mpya ya kielezo cha hivi punde cha Thamani ya Nyumba kutoka kampuni ya CoreLogic, ina onesha ongezeko katika kila mji mkuu isipokuwa Hobart. Bei katika maeneo ya kanda katika majimbo yote nchini zili ongezeka.

Utawala wa kijeshi nchini Burma umetangaza wiki ya moja ya maombolezo ya kitaifa Jumatatu, Machi 31, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi siku ya Ijumaa lililoua zaidi ya watu 1,700 nchini humo na nchi jirani ya Thailand.

Burkina Faso, Mali na Niger zimeamua kuanzisha ushuru wa forodha wa pamoja wa 0.5% kwa bidhaa wanazoagiza kutoka nchi zilizo nje ya shirikisho lao ili kufadhili shughuli zao. Inayoitwa "tozo ya shirikisho la AES", hii haipaswi, hata hivyo, kuathiri bidhaa kutoka nchi za WAEMU, ambazo Ouagadougou, Bamako na Niamey bado ni wanachama, ingawa zlijiondoa katika ECOWAS mnamo mwezi wa Januari.

Serikali ya Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo, inarejelea mashauriano ya kitaifa ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, yaliyoanza wiki moja iliyopita, na kususiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa wa upinzani. Mashauriano haya yanayoongozwa na kamati maalum inayomshauri rais Tshisekedi kuhusu masuala ya usalama, yanatarajiwa kumalizika wiki hii.

Share