Taarifa ya Habari 25 Machi 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi Richard Marles, amesema kutakuwa uwekezaji wa ziada katika idara ya Ulinzi wa dola bilioni 1 katika bajeti itakayo tangazwa usiku wa leo Jumanne Machi 25.


Waziri Mkuu Anthony Albanese amekaribisha majimbo yote na wilaya zote, baada mamlaka hizo kutia saini makubaliano ya uwekezaji wa shule ya Serikali ya shirikisho.

Wakuu wa nchi toka jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya maendeleo ya kusini mwa Afrika, SADC, watakutana hivi leo kwa njia ya mtandao, kujadiliana kuhusu hali inayoendelea mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Vijana nchini Kenya, Jumatatu waliandamana nje ya jengo ambalo mahojiano ya kumteua mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) yalikuwa yakiendelea huku wakidai kuwa baadhi ya walioteuliwa walikuwa wazee.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share