Taarifa ya Habari 10 Disemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri wa Huduma za Serikali Bill Shorten ametangaza kuwa shirika la Services Australia, lime tekeleza karibu nusu ya mapendekezo yote kutoka Tume yakifalme kwa mfumo usio halali wa Robodebt.


Mpango huo waki dijitali, ulio endeshwa na serikali kadhaa za mseto kuanzia mwaka wa 2016 hadi 2020, ulisababisha wa madeni ya uongo kutolewa kwa wa Australia 470,000 na serikali ya shirikisho. Bw Shorten ame ongezea kuwa mapendekezo 25 kati ya 26 kwa idara yake, yame tekelezwa na pendekezo moja la mwisho linalo husiana na ofisi ya kodi ya Australia, liko katika mchakato waku tekelezwa kwa sasa.

Wasafiri mjini Sydney wame kabiliana na kuchelewa kwa treni Jumatatu 9 Disemba licha ya mafanikio ya dakika ya mwisho yaku zuia mgomo wa wafanyakazi wa usafiri wa New South Wales. Migomo ilikuwa imepangwa kwa jana Jumatatu na katika mwezi mzima wa Disemba baada ya mashauriano kuhusu mishahara na serikali ya jimbo kufeli tena. Chama hicho cha wafanyakazi kime dai nyongeza ya mshahara ya asilimia 32 kwa muda wa miaka minne, kwa upande wayo serikali inapendekeza kutoa asilimia 9.5 katika muda wa miaka mitatu.

Data mpya inaonesha kuwa mwaka wa 2024 utakuwa mwaka mwenye joto zaidi duniani tangu mwanzo wa kumbukumbu, na nyuzi joto za juu zinatarajiwa kuendelea hadi katika miezi michache ya kwanza ya 2025. Matokeo kutoka uchunguzi wa shirika la Copernicus Climate Change Service la Muungano wa Ulaya, yame jiri wiki mbili baada ya mazungumzo ya mazingira ya Umoja wa Mataifa kutoa makubaliano ya $469 bilioni za Austrlaia zaku kabiliana na mabadiliko ya mazingira. Ni mwaka wa kwanza ambako nyuzi joto wastan duniani zimepita digri 1.5 juu ya 1850-1900 kiwango cha kipindi cha kabla ya viwanda. Kikomo muhimu ambacho nchi zilikuwa zime ahidi kuepuka katika makubaliano muhimu ya Paris ya 2015.

Mapigano yameendelea kuripotiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23, huku maelfu ya watu wakiyakimbia mapigano hayo yaliyokatiza safari za barabara ya Gomba-Butembo. Vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa mapigano hayo ya jana Jumapili yamezuka baada ya utulivu ulioonekana Jumamosi jioni katika vijiji vya Luofu, Miriki na Matembe ambako jeshi la Kongo lilishambuliwa kwa mizinga na waasi wa M23 wanaodaiwa kusaidiwa na jeshi la Rwanda. Milio ya mabomu na silaha nzito yamesababisha hofu kubwa kwa wakaazi walioanza kuhangaika kwa wiki moja sasa.

Rais William Ruto na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta wanasemekana kuanzisha mazungumzo katika kile kinachoonekana kama jaribio la kiongozi wa taifa kupunguza uasi dhidi yake, haswa katika eneo la Mlima Kenya. Duru zimeambia Taifa Leo kwamba, Rais Ruto pia anajaribu kuridhiana na wandani wake wa zamani ili kuongeza uthabiti katika serikali ya Kenya Kwanza. Ushawishi wa Rais Ruto umeshuka zaidi katika Mlima Kenya kwa sababu wakazi wamekasirishwa na hatua yake ya kufanikisha kutimuliwa kwa aliyekuwa naibu rais, Bw Rigathi Gachagua.

Wakati Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA kikijiandaa na uchaguzi mkuu wa Taifa wa chama hicho, tayari zimeibuka taarifa za baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho kutaka kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Taifa. Wadhifa huo umekuwa ukishikiliwa na mwenyekiti wa sasa Freeman Aikael Mbowe kutoka mwaka 1995 huku taarifa hizo za baadhi ya wanachama kutaka kurithi mikoba ya Mbowe, zikitafisiriwa kama mpasuko ndani ya chama hicho na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na baadhi ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii nchini Tanzania wanaona kama Lisu atajitokeza kupambana na Mbowe itakuwa ni kipimo sahihi cha Demokrasia ndani ya CHADEMA.

Share