Zaidi ya nyumba 230,000 na biashara zimesalia bila umeme katika majimbo yote mawili. Christie Johnson ni mtabiri wa hali ya hewa mwenye cheo kikuu katika shirika la Utabiri wa Hewa. Alipo zungumzia tukio hilo alisema mvua nzito inatarajiwa kupungua mchana wa leo ila, hatari ya mafuriko ina tarajiwa kupungua mchana wa leo ila, hatari ya mafuriko inatarajiwa kuendelea hadi katikati ya wiki hii kwa sababu ya ongezeko ya viwango vya maji katika mifumo wa mto. Wakati huo huo mamlaka wana wahamasisha watu waepuke kuendesha magari katika maji ya mafuriko.
Kwa upande wake kiongozi wa jimbo la New South Wales, Chris Minns amesema mamlaka walijitayarisha vizuri zaidi kwa jibu lao la kutuma rasilimali Lismore, mji ambao una kabiliana na tukio lingine la mafuriko, miaka mitatu baada ya tukio la mwisho kama hilo. Jumapili, onyo za mafuriko makubwa zilipunguzwa wakati viwango vya maji katika mto Wilson, kupungua na onyo zakuhama kwa mji wa Lismore zili ondolewa, nakuwaruhusu wakaaji kurejea nyumbani kwao kwa tahadhari.
Kiongozi wa chama cha Greens cha WA Brad Pettitt, amesema chama chake kiko katika nafasi nzuri yaku shikilia usawa wa mamlaka ndani ya nyumba ya juu ya bunge la jimbo hilo. Chama cha Labor kilishinda uchaguzi mkuu wa jimbo hilo kwa urahisi kwa muhula wa tatu, hatakama wame athirika kwa kupoteza asilimia 18 ya uvutio wa kura, wapiga kura wengi waki unga mkono vyama vidogo pamoja na wagombea huru. Bw Brad Pettitt ameongezea kuwa chama chake kimepokea, kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa jimbo hilo.
Marekani imewaamuru wafanyakazi wake wasiohusika na shughuli za dharura za serikali kuondoka Sudan Kusini kwa sababu za kiusalama. Imesema mapigano yanaendelea nchini humo yakihusisha makundi mbalimbali. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema makundi yanayohusika katika mapigano ya sasa ni ya kisiasa na kikabila. Imeongeza kuwa tayari silaha zimeshaufikia umma.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza zawadi ya Dola Milioni tano, kwa yeyote atakayesaidia ukamataji wa viongozi wa kundi la waasi M23, ambao wameongoza wapiganaji wake kuchukua miji ya Goma na Bukavu, Mashariki mwa nchi hiyo. Wizara inayoshughulikia masuala ya Haki nchini humo imesema kitita hicho cha fedha kitakabidhiwa kwa yeyote, atakayesaidia kukamatwa kwa , na . Kinshasa, inasema yeyote akayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukamatwa kwa viongozi hao watatu, ambao wote walifunguliwa mashtaka mwezi Agosti mwaka 2024 bila uwepo wao na kuhukumiwa kifo.
Katika michezo: Katika mchezo wa Gofu, mu Australia Karl Vilips anasherehekea ushindi wake wa kwanza wa PGA, kupitia ushindi wake katika michuano ya wazi ya Puerto Rico. Hii ni mara yake ya nne kuanza katika michuano ya PGA. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 ni mchezaji wa 12 kuwahi kushinda mchuano wa PGA mapema sana katika mchezo huo. Matokeo hayo yame mweka katika michuano yamabingwa wiki ijayo na michuano ya PGA itakayo kuwa Mei, pamoja na kusamehewa kushiriki kwa miaka mbili katika ziara ya PGA. Alishinda mashindano yadunia ya gofu ya watoto nchini Marekani mara mbili, na mashindano ya vijana ya dunia ya Callaway akiwa na miaka 10 na 12.]] Vilips amesema ni ndoto iliyo timia. Katika, Novak Djokovic amesema anafanya awezavyo kuvumilia, baada ya kuondolewa mapema katika mchuano wa BNP Paribas Open wa Indian Wells. Bingwa huyo maratano katika michuano ya Indian Wells, alipoteza katika seti tatu dhidi ya mchezaji mwenye ubora wa 85 katika orodha ya wachezaji bora duniani Botic Van De Zandschulp [[6-2, 3-6, 6-1]] katika raundi ya pili ya mchuano huo. Djokovic amesema alikuwa na wakati mgumu kupata mdundo sahihi katika mchezo huo. Wakati huo huo, Mchezaji kutoka Australia ambaye ni namba 10 kwa wachezaji bora duniani, Alex de Minaur, ambaye amepewa nafasi ya tisa katika mashindano hayo, alipata ushindi waku sisimua wa seti mbili sufiri dhidi ya mveterani mubelgiji David Goffin katika jangwa la California Jumapili.