Bi O’Neil amesema mapokezi yatapunguzwa kwa idadi yawa hamiaji 185,000 wachache katika muda wa miaka minne wa bajeti. Uhamiaji wa ng’ambo ulifikia kilele wakati wa mwaka wa fedha wa mwisho ambapo idadi ya watu 500,000 wali wasili nchini Australia, hali ambayo ni tofautia kufuatia miaka mbili ya mipaka kufungwa wakati wa uviko. Bi O'Neil ame ongezea kuwa mapokezi hayo yata fikiwa kwa kukaza masharti ya viza, yanayo jumuisha kupunguza muda wa viza za wahitimu. Wakati huo huo, katibu wa shirika la Unions NSW, Mark Morey, amesema anakaribisha mageuzi ambayo yata fanya iwe rahisi kwa wafanyakazi ambao ni wahamiaji kuondoka katika mazingira ambako wana nyanyaswa na waajiri, pamoja nakusafisha njia kwa makazi yakudumu ila, ameongezea kuwa vizuizi kwa masaa ya wafanyakazi ya wanafunzi wakimataifa yanastahili ongezwa.
Wakati nchi zinazo shiriki katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa wanapo endelea kutofautiana kuhusu kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, kundi la nchi zinazo ongozwa na Denmark lime amua kuunda lengo kuu la: kuondoa hewa chafu zaidi kutoka mazingira kuliko wanayo zalisha. Kundi la wazalishaji hewa hasi, lime zinduliwa na Denmark, Finland na Panama na lina lengo la kufikia lengo hilo kwa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu pamoja naku panua misitu na kuwekeza katika teknolojia mpya. Panama tayari imefikia lengo hilo, kupitia misitu yake mikubwa inayo tumika kama shimo kubwa lakuzamisha kaboni. Finland na Denmark zinatumai kufikia malengo hayo kufikia 2035 na 2045 mtawalio.
Kanda la kaskazini Queensland lina jiandaa kwa ujio wa Kimbunga cha tropiki Jasper Jumatano. Waaji kati ya mji wa Cape Melville, katika pwani ya mashariki ya Cape York Peninsula, na Townsville zime wekwa chini ya onyo kuwa pepo kali ya uharibifu pamoja na uwezekano wa mafuriko yana elekea wanako ishi. Wameonywa kuwa miti na nyaya za umeme huenda zika angushwa, na paa zinaweza rushwa kutoka nyumba pamoja na kitu chochote ambacho hakija fungwa chini. Shirika la moto na dharura ya Queensland, limesema umeme, simu pamoja na huduma za intanet zinatarajiwa kupotezwa pamoja na upatikanaji wa maji, utavurugwa kwa sababu ya mwelekeo wa sasa wa kimbunga hicho. Ongezeko ya dhoruba itakuwa na maana ya uwepo wa mafuriko katika baadhi ya sehemu na jamii kutengwa.
Wakaaji katika moja wa mji mkuu wa kusini Gaza, Khan Younis wamesema magari yajeshi ya Israel yamefika katika barabara kuu ya kaskazini kusini katika mji huo.
Vita vikali katika masaa 24 yaliyo pita, imepunguza kasi ya vikosi vya Israel kutoka eneo la mashariki. Takriban 90% ya wakaaji wa Gaza ambao ni milioni 2.3 wame tawanywa ndani ndani ya eneo hilo ambalo mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema hakuna sehemu salama yaku kimbilia.
Kukatika kwa umeme kulianza saa mbili usiku kwa saa za huko, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa umeme kukatika nchini humo, ndani ya miezi mitatu iliyopita. Kenya ilikumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme nchi nzima Jumapili jioni, na kupelekea shughuli kusimama sehemu kubwa za nchi, ikiwa ni pamoja na uwanja mkuu wa ndege katika mji mkuu, Nairobi, kituo kikuu cha usafiri kinachounganisha Afrika Mashariki na Asia, Ulaya na sehemu nyingine za dunia. Kukatika kwa umeme kulianza saa mbili usiku kwa saa za huko, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa umeme kukatika nchini humo, ndani ya miezi mitatu iliyopita. Miongoni mwa vituo muhimu vilivyoathiriwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, pamoja na Uwanja wa Ndege wa Eldoret magharibi mwa Kenya, ambapo jenereta za umeme za dharura zilishindwa kufanya kazi, baada ya umeme wa gridi ya kitaifa kufeli.
Viongozi wa Afrika Magharibi walikutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, leo kwa mazungumzo ya kanda yao katika mgogoro unaozidi kuongezeka baada ya nchi nne kuangukia katika utawala wa kijeshi na hatari zinazoongezeka kutokana na migogoro ya makundi yenye msimamo mkali ya Sahel. Baada ya mapinduzi ya Mali, Burkina Faso, Guinea na Niger kuanzia 2020, jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), imeshuhudia wanachama wake Sierra Leone na Guinea-Bissau zikiripoti majaribio ya mapinduzi katika wiki za hivi karibuni. Kujiondoa kwa jeshi la Ufaransa, Sahel, kanda ya jangwa la Sahara, kote barani Afrika, kumeongeza wasiwasi juu ya migogoro inayoenea kusini mwa mataifa ya Ghuba ya Guinea, Ghana, Togo, Benin na Ivory Coast. Tahadhari ya kimataifa imeangazia mapinduzi ya karibuni ya Niger, na kusababisha ECOWAS kuweka vikwazo vikali na kufunga biashara.
Na katika michezo, nyota wa soka wa Australia na timu ya wanawake ya Chelsea Sam Kerr, amepokea kipigo kutoka kwa timu ya wanawake ya Arsenal katika ligi kuu ya Uingereza. Arsenal ilishinda mechi hiyo kwa magoli 4-1 na timu hiyo ilikuwa na wachezaji kadhaa wa timu ya taifa Australia kama Steph Catley, Caitlin Foord na Kyra Cooney-Cross. Ushindi huo ume ifikisha Arsenal katika kilele cha ligi hiyo ambako ina alama 22 sawia na Chelsea ila Arsenal imefunga goli nyingi zaidi.