Taarifa ya habari 11 Machi 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Mamlaka jimboni New South Wales wamesema jibu baada ya kimbunga Alfred lime hamia rasmi katika mwelekeo wa uokoaji. Hakuna onyo za dharura ambazo zimetolewa kwa kuhama.


Viwango vya maji vina pungua na huduma za dharura za jimbo zita ondoa tangazo za kuhama, nakuwashauri wakaaji kuwa wanaweza rejea kwa tahadhari. Jumuiya ya Waislamu wa Queensland lime chukua hatua ya kuwasaidia wakaaji baada ya tukio la kimbunga cha kitropiki Alfred, ofisi ya utabiri wa hewa ikionya mifumo ya mito bado inakabiliwa kwa ongozeko ya viwango vya maji jimboni Queensland na kaskazini New South Wales. Syed Asghar Naqvi ni Rais wa Shirika la Pakistan Australian Cultural Association of Queensland. Amesema misikiti imekuwa ikitoa makaazi kwa wanao hitaji, wakati watu wakujitolea ndani ya jumuiya wana toa vifurushi vya vyakula.

Kiongozi wa chama cha Greens cha WA Brad Pettitt, amesema chama chake kiko katika nafasi nzuri yaku shikilia usawa wa mamlaka ndani ya nyumba ya juu ya bunge la jimbo hilo. Chama cha Labor kilishinda uchaguzi mkuu wa jimbo hilo kwa urahisi kwa muhula wa tatu, hatakama wame athirika kwa kupoteza asilimia 18 ya uvutio wa kura, wapiga kura wengi waki unga mkono vyama vidogo pamoja na wagombea huru. Chama cha Liberal cha Magharibi Australia, kimesema kina zingatia hatma yake kufuatia ushindi wa pili mfululizo wa chama cha Labor katika uchaguzi wa jimbo hilo. Kiongozi wa chama cha Liberal jimboni humo Libby Mettam ame dokeza kuwa ata endelea katika wadhifa huo, akisema Jumapili kuwa ata achia chama chake uamuzi huo. Hesabu mpya kutoka uchaguzi wa Jumamosi umeonesha kuwa chama cha Labor kilishinda viti 41, hali ambayo imekipa chama hicho ushindi mkubwa dhidi ya upinzani wa mseto.

Vuguvugu la waasi na kijeshi la AFC-M23 linaendelea kusonga mbele. Baada ya siku nne za mapigano dhidi ya jeshi la Kongo na makundi yenye silaha yanayounga mkono majeshi ya serikali ya FARDC, vuguvugu la kisiasa na kijeshi linaloungwa mkono na Rwanda limechukua udhibiti wa Nyabiondo, eneo lililo katika eneo la Masisi, zaidi ya kilomita mia moja kutoka Goma. Mafanikio haya mapya ya AFC-M23 huko Nyabiondo sasa yanafungua njia hadi Walikale, eneo lenye utajiri wa madini, hivyo kuongeza shinikizo kwa Wanajeshi wa Kongo (FARDC). Mvutano tayari umeonekana tangu Januari katika eneo hili la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, takriban raia wanne waliuawa katika mapigano katikati mwa Masisi, inayoshikiliwa na AFC-M23.

Kufuatia wito wa Rais Salva Kiir siku ya Ijumaa, Machi 7 kutakakuwataka raia kuwa na utulivu, mashirika ya kiraia nchini Sudani Kusini yanasema yana wasiwasi mkubwa kuhusu kuzuka upya kwa ghasia katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo, hasa katika Jimbo la Upper Nile, na kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa kisiasa.

Kinara wa ODM Raila Odinga Jumapili alikumbana na ghadhabu za Wakenya ambao hawajafurahishwa na hatua yake ya kuhalalishwa uhusiano wake wa kisiasa na Rais William Ruto. Siku mbili tu baada ya kutia sahihi mkataba wa kisiasa na Rais Ruto, mwanasiasa huyo mkongwe, jana alizomewa vikali na vijana alipojiunga nao katika kaunti ya Kisii. Haya yalikuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa sare mpya za timu ya Shabana, inayoshiriki ligi kuu ya kitaifa (FKF-PL) katika uga wa Gusii. Vijana hao walimpigia mayowe Bw Odinga kwa kipindi kirefu alichokuwa uwanjani humo, wakitoa kauli za “Ruto Must go! Raila must go!”

Share