Wakati huo huo chama cha Greens kime kosoa mkakati mpwa wa serikali kikisema chama cha Labor kina laumu kimakosa wahamiaji kwa mgogoro wa makaazi. Jana jumatatu serikali iliweka wazi mageuzi yake kwa mfumo wa uhamiaji, kwa kutangaza mipango yakupunguza kwa nusu uhamiaji wa jumla kaitka miaka mbili ijayo, wakati inavutia wafanyakazi wengi mhimu wenye ujuzi wa juu katika muongo ujao.
Maelfu ya wakaaji wa Kusini Australia wame achwa bila umeme, wakati upepo mkali ume lazimisha shule kadhaa pamoja na baadhi ya hospitali ziki tumia jenereta za akiba. Shirika la huduma ya dharura ya jimbo hilo SES, limejibu wito wa kazi 900 jimboni kote, nyingi ya kazi hizo ziki husu uharibifu ulio sababishwa na miti iliyo anguka, pamoja na mawe makubwa na upepo wa kasi ya kilomita 90 iliyo rekodiwa katika baadhi ya sehemu ya jimbo hilo.
Waziri wa Afya Shannon Fentiman ame ondoa ugombea wake kuwa kiongozi wa Queensland, hatua hiyo ina maana Naibu kiongozi wasasa Steven Miles ndiye atakaye rithi mikoba ya uongozi wa jimbo hilo. Hatua hiyo imejiri baada yamakubaliano kufikiwa kati ya Bw Miles na mweka hazina wa Queensland Cameron Dick, akitarajiwa kuwa Naibu kiongozi wa jimbo hilo.
Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa anahangaika siku ya Jumatatu kutafuta kura za kutosha kwa ajili ya sera yake uhamiaji ya kuwapeleka wanaoomba hifadhi nchini Rwanda baada ya wabunge wa chama chake kusema mpango wa sheria ya dharura hauna nguvu ya kutosha. Sunak anakabiliwa na mtihani muhimu kwa utawala wake, wakati wanasiasa wa mrengo wa kulia na kushoto wa chama cha Conservative wakitishia kuupinga mswaada huo hiyo wakati utakapofikishwa bungeni siku ya Jumanne.
Watu wawili wameuwa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulizi kwa msafara wa kibinadamu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ICRC imesema Jumapili. Waliojeruhiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu wa ICRC, Shirika la Msalaba Mwekundu limesema katika taarifa yake.
Shirika la ndege la Kenya la Kenya Airways, limewaambia wateja wake kuhusu uwezekano wa kuvurugika kwa baadhi ya safari zake wakati wa msimu wa sikukuu ya Krismasi kutokana na uhaba wa vipuri. Shirika hilo ambalo ni moja ya mashirika makubwa sana ndege barani Afrika, limesema kwamba uhaba huo ambao unashuhudiwa kote ulimwenguni utaathiri safari zake kwa takriban wiki mbili.