Taarifa ya Habari 12 Juni 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Bill Shorten akosoa usimamizi wa mfumo wa N-D-I-S akisema, ni jinamizi la ukiritimba na ame ahidi kurejesha imani tena kwa NDIS


Waziri wa ulinzi Richard Marles anamatumaini anaweza anzisha mazungumzo, na waziri mwenza wa China anapo hudhuria kongamano lakimataifa nchini Singapore. Kume kuwa wasiwasi kuhusu kisa kati ya ndege ya udukuzu ya manamaji wa Australia, pamoja na ndege yakivita ya China katika eneo la bahari lakusini ya China mwezi uliopita.

Tanzania imetiliana saini mkataba wa gesi na kampuni za Shell ya Uingereza na Equinor ya Norway ili kuutekeleza mradi wa dola bilioni 30 wa kuiwezesha nchi hiyo ya Afrika mashariki kuuza gesi yake asilia. Kulingana na mkataba huo uwekezaji kwa ajili ya mradi huo utakamilishwa mnamo mwaka 2025 na kuanza shughuli kati ya mwaka 2029 na 2030 kwenye mtambo wa gesi ya kioevu utakaojengwa katika mji wa Lindi kusini mwa Tanzania.

Rwanda iko katika hali ya utata ikiwa inakaribia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Viongozi wa Serikali wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliondaliwa kufanyika wiki ya Juni 23, wakati ikikabiliana na tuhuma mfululizo za jirani yake kuhusu kuingilia nchi hiyo. Wakati matayarisho yakiwa yameshika kasi kabla ya mkutano huo, mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo (DRC) unaweka dosari kabla ya tukio hilo, ukiwasukuma maafisa wa serikali kukanusha madai ya kuwa Kigali ina jukumu fulani katika ghasia mpya zinazoendelea. Kigali imekanusha na kutupilia mbali shutuma hizo.


Share