Ripoti hiyo imeonesha kuwa Wanawake waislamu pamoja na wasichana wali lengwa katika asilimia 60 ya mashambulizi yakimwili, asilimia 79 katika mashambulizi ya maneno pamoja na matukio yote yaku temewa mate, takriban yote yaliyo fanywa na wanaume. Data hiyo ilichukuliwa kutoka mamia ya ripoti zilizofanywa kwa sajili ya unyanyasaji wa waislamu ya Australia na, ilikusanywa na watafiti wa Monash ambao walifanyia tafiti machapisho elfu 18 katika mtandao wakijamii wa X.
Kiongozi wa jimbo la New South Wales Chris Minns, ametetea uamuzi wa serikali yake waku bomoa nyumba zilizokuwa tupu, zilizo haribiwa na maji katika mji wa Lismore ambako, watu wasiokuwa na makaazi wame kuwa waki ishi wakati wa mafuriko yaliyo sababishwa na kimbunga chaki tropiki cha zamani Alfred. Nyumba hizo za kaskazini New South Wales zili nunuliwa na serikali baada ya mafuriko mabaya ya 2022, kwa sababu zilizingatiwa kuwa hatari. Wanao ishi katika nyumba zilizo katika mtaa wa Pine, wamesema watapinga amri zaku hama ila, Bw Minns ame sisitiza kuwa watu hao wanaweka maisha yao na yale ya watu wakujitolea kutoka huduma ya dharura ya jimbo hatarini.
Jumuia ya maendeleo ya Afrika Mashariki Jumatano ilionya kwamba mapigano ya hivi karibuni nchini Sudan Kusini yanaipeleka nchi hiyo “kwenye hatari ya kurudi katika vita.” Kupitia historia yake fupi, taifa hilo maskini limekumbwa na na mzozo wa kisiasa na ukosefu wa usalama, lakini wasiwasi uliongezeka hivi karibuni baada ya mapigano kati ya majeshi washirika kwa viongozi hasimu wa nchi hiyo. Rais Salva Kiir aliapa kwamba nchi haiwezi kurejea katika vita, lakini mapigano hayo yalitishia makubaliano ya 2018 ya kushirikiana madaraka ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano kati yake na Makamu wa kwanza wa Rais Riek Machar.
IGAD ilisema ghasia hizo ni za hivi karibuni katika msururu wa matukio “yanayoipeleka Sudan Kusini kwenye hatari ya kurudi katika vita”.
Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yataanza katika mji mkuu wa Angola tarehe 18 Machi, ofisi ya rais wa Angola ilisema Jumatano katika taarifa. Taifa hilo la kusini mwa Afrika limekuwa likijaribu kuwa mpatanishi ili kufikia sitisho la mapigano la kudumu na kupunguza mvutano kati ya Congo na jirani yake Rwanda, ambayo imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono M23.
Rwanda inakanusha madai hayo.
Shirika la riadha la Australia lime tangaza wanariadha 20 bingwa wa dunia, washindi wa medali katika olimpiki pamoja na nyota chipukizi watakao shiriki katika michuano ya 2025 ya ndani ya dunia nchini China. Bingwa mtetezi na mshindi mara mbili wa medali ya fedha Nicola Olyslagers, ata rejea katika jukwaa la ndani kutetea taji lake laku ruka.
Ata ungwa na mshindi wa medali ya fedha na bingwa wa dunia wa 2022 Eleanor Patterson. Michuano hayo ita peperushwa mubashara katika runinga ya SBS VICELAND na SBS On Demand kuanzia tarehe 21 hadi 23 Machi.