Taarifa ya Habari 14 Agosti 2023

City - Swahili.jpg

Wazazi wa mwomba hifadhi kutoka Iran aliye uawa wakati wa mgomo katika kisiwa cha Manus mnamo 2014, wamefikia suluhu ya siri na serikali ya shirikisho pamoja na kampuni ya ulinzi ya G4S.


Reza Barati alipigwa hadi kufa na walinzi pamoja na wakandarasi wengine wakati wa mgomo katika kizuizi cha ng’ambo kilicho kuwa kikisimamiwa na Australia mnamo Februari 2014. Familia yake alifungua mashtaka dhidi ya serikali katika mahakama kuu ya Victoria, miaka mbili iliyopita. Mwanasheria Jennifer Kanis aliyewakilisha familia ya Reza Barati, amesema suluhu hiyo haijumuishi kukiri wa kwajibu kutoka kwa serikali ya Australia.

Ripoti mpya imebaini kuwa wafanyakazi mhimu wanatumia hadi 70% ya mishahara yao kwa kodi. Ripoti hiyo imepata kuwa walimu wa elimu ya mapema ya watoto, wauguzi, pamoja na wafanyakazi katika huduma za malezi ya wazee wa muda wote, wanaweza mudu tu, nyumba moja kati ya nyumba 100 zakukodi. Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Anglicare Australia Kasy Chambers, amesema hali hiyo ni tata haswa kwa wafanyakazi hao mhimu. Mamlaka jimboni Hawaii wanafanya uchunguzi kubaini kama, mengi zaidi yangefanywa kuwaonya wakaazi wa kisiwa cha Maui katika masaa kabla ya moto mubaya wa vichaka kukabili eneo hilo. Mioto hiyo iliteketeza Kijiji kizima cha Laihaina [[la-HIGH-nah]] na imethibitishwa kuwa watu 93 walifariki na mamia haijulikani waliko.

Polisi nchini Tanzania wamewakamata wakili mmoja na mwanasiasa wa upinzani, wakiwahutumu kwa kuchochea na kupanga maandamano kote nchini humo kwa lengo la kuiangusha serikali. Wakili Boniface Anyasile Mwabukusi na Mpaluka Nyagali walikamatwa jumamosi. Wakili Mwabukusi, alikuwa miongoni mwa mawakili waliowasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba huo, na kesi ilitupiliwa mbali alhamisi wiki iliyopita. Amesema atakata rufaa. Wakili wa wawili hao, Philip Mwakilima, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba alikuwa anafanya kila juhudi kuzungumza na wateja wake wanaozuliwa na polisi, na kwamba madai dhidi yao ni ya uongo.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS imeendeleza juhudi zake za kutafuta njia za kidiplomasia za kubatilisha mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Niger mwezi uliopita. Juhudi hizo zinafanyika wakati ikiiendeleza msimamo wake wa kutishia kuingilia kati kijeshi kwenye taifa hilo katika mzozo huo mkubwa uliozivuta nchi zenye nguvu duniani. Jumuiya hiyo, jana Jumamosi ilisema kwamba imedhamiria kutuma kamati ya bunge ili ikutane na viongozi wa mapinduzi ambao wanamshikilia Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, na wameshavunja serikali yake. Mapinduzi ya kijeshi ya Niger ni ya saba Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kati katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika michezo, uwezekano wakuwa na likizo ya umma kuenzi mafanikio ya Australia katika kombe la dunia, unaendelea kukaribia baada ya Waziri mkuu kuongeza sauti yake kwa wito wa sherehe yakitaifa.
Matildas walikita katika nusu fainali baada yakushiriki katika mikwaju ya penati yakusisimua dhidi ya Ufaransa, hatua ambayo inawakutanisha na Uingereza jumatano.
Wenyeji wakishinda nakuingia katika fainali na washinde fainali hiyo pia, Waziri Mkuu Anthony Albanese amependekeza uwezekano wa wafanyakazi nchini kupewa likizo ya umma kuenzi ushindi huo.


 




Share