Taarifa ya Habari 14 Machi 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Wauguzi na wakunga wanaomba mageuzi ya udhibiti yatakayo waruhusu kuagiza vipimo vya uchunguzi, kutoa rufaa kwa watalaam na kuagiza dawa fulani. Ni hatua mashirika ya kilele yamesema itapunguza muda wakusubiri nakupiga jeki matokeo ya huduma ya afya.


Seneta wa chama cha Greens Mehreen Faruqi ame mwandikia Waziri Mkuu Anthony Albanese, akiomba hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na ongezeko ya unyanyasaji dhidi ya waislamu nchini Australia. Seneta Faruqi alikosoa anacho ita "mtazamo wa upande mmoja kwa ubaguzi wa rangi" wa serikali, akisema "amekerwa na uhaba wa haraka kutoka kwa serikali yako kushughulikia unyanyasaji dhidi ya waislamu, dhidi ya wa arabu na ubaguzi dhidi yawa Palestina. Waandishi wa ripoti hiyo waliwasilisha mapendekezo 28, yanayo jumuisha kuwekeza kwa msaada wakisaikolojia ya waathirika, elimu kwa jumuiya na kutoa mafunzo kuhusu mikakati ya kukabiliana.

Kiongozi wa jimbo la New South Wales Chris Minns, ametetea uamuzi wa serikali yake waku bomoa nyumba zilizokuwa tupu, zilizo haribiwa na maji katika mji wa Lismore ambako, watu wasiokuwa na makaazi wame kuwa waki ishi wakati wa mafuriko yaliyo sababishwa na kimbunga chaki tropiki cha zamani Alfred. Nyumba hizo za kaskazini New South Wales zili nunuliwa na serikali baada ya mafuriko mabaya ya 2022, kwa sababu zilizingatiwa kuwa hatari.

Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimesema kinafanya uchunguzi wa kina ili kubaini kiwango cha maambukizi ya homa ya nyani (MPOX) na kinatarajia kutoa ripoti rasmi wiki ijayo. Taarifa hiyo imekuja siku chache baada ya Tanzania kuripoti visa viwili vya MPOX miongoni mwa raia wake, huku kukiwa na madai ya uwezekano wa idadi kubwa zaidi ya wagonjwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yataanza katika mji mkuu wa Angola tarehe 18 Machi, ofisi ya rais wa Angola ilisema Jumatano katika taarifa. Taifa hilo la kusini mwa Afrika limekuwa likijaribu kuwa mpatanishi ili kufikia sitisho la mapigano la kudumu na kupunguza mvutano kati ya Congo na jirani yake Rwanda, ambayo imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono M23.
Rwanda inakanusha madai hayo. Angola ilitangaza Jumanne kwamba itajaribu kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja.

Waandishi wa habari kadhaa wamepigwa, kukamatwa, na vifaa vyao kuharibiwa na vikosi vya usalama walipokuwa wakiripoti uchaguzi mdogo uliogubikwa na ghasia hii leo.
Viongozi wa mashirika ya wanahabari nchini pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari wamelaani vikali vitendo hivyo, wakitaka serikali iwajibike kwa hujuma, hasara, na udhalilishaji uliotekelezwa na vyombo vya usalama. Baadhi ya wadau wanadai kuwa hujuma hizi dhidi ya wanahabari huenda zimechochewa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwanawe Rais Yoweri Museveni.

Share