Takriban idadi yawatu elfu moja wanao ishi katika mji wa Forbes jimboni New South Wales, wame ambiwa waondoke mjini humo kwa sababu ya matarajio ya mafuriko makubwa, na eneo lote la katikati magharibi limewekwa katika tahadhari ya juu.
Takriban wanajeshi 100 wa jeshi la ulinzi wame tumwa mjini humo, kusaidia katika oparesheni za uokoaji. Msaada pia unapelekwa mjini humo kutoka New Zealand, watu 12 wakujitolea wanawasili mjini humo pamoja na ndege 14 za uokoaji, na zingine 4 ambazo zitasaidia katika maswala ya usafiri na vifaa.
Kiongozi wa jimbo la Magharibi Australia, ametetea matendo ya kituo cha kizuizi cha vijana cha Perth, licha ushahidi ambao umeibuka kuhusu vizuizi vyenye madhara vinavyo tumiwa dhidi ya watoto. Video iliyo oneshwa kwenye makala ya Four Corners ya runinga ya ABC jana Jumatatu, imeonesha kijana mmoja akihudumiwa kikatili kwa kutumia mbinu yaku kunja, ambayo ingesababisha kuzimia au kifo.
Bunge la Tanzania lilipitisha Mswaada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi mwaka 2022, mapema mwezi Novemba na sasa unasubiri saini ya Rais ili kuwa sheria. Mswaada huo unaweka mazingira magumu kwa mtu yeyote anayekusanya taarifa binafsi nchini Tanzania na pia unatoa mamlaka makubwa kwa tume ya kusimamia utekelezaji wake. Unaweka mazingira magumu kwa wanaokusanya taarifa binafsi nchini Tanzania kuzisafirisha nje ya nchi, pamoja na kutoa adhabu kali ya hadi shilingi milioni 100 na kifungo cha miaka 2 gerezani kwa yeyote atakayekiuka mswaada huo utakapoidhinishwa na kuwa sheria.
Marekani imesema itatoa zawadi ya hadi dola milioni 10 kwa yeyote ambaye atakuwa na taarifa kuhusu viongozi wakuu wa Al-Shabab. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza kuwa, kwa mara ya kwanza itatoa donge nono kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa itakayowezesha kusaidia kutatiza mifumo ya kifedha ya kundi la Al-Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda.