Waziri Mkuu Anthony Albanese hii leo Alhamisi 20 Februari, ame enda Whyalla Kusini Australia, kutangaza mfuko wa msaada wa kiwanda, siku moja baada ya serikali ya Kusini Australia kiwanda cha vyuma vya mji huo chini ya usimamizi.
Kiongozi wa jimbo la Kusini Australia Peter Malinauskas atakuwa huko pamoja na Bw Albanese na ameharakisha kupitisha sheria husika ndani ya bunge la jimbo hilo.
Thamani ya nyumba katika maeneo ya kanda, imeongezeka kuliko thamani ya nyumba ambazo ziko katika miji mikuu. Miji kama Gladstone, Townsville, na Mackay jimboni Queensland, na Bunbury pamoja na Busselton katika jimbo la Magharibi Australia, ime ongeza takriban $100,000 kwa bei ya kati ya nyumba katika mwaka ulio pita.
Sudan inamshutumu Rais William Ruto wa Kenya kwa kukiuka ahadi katika ngazi ya juu kabisa, ikidai kuwa Kenya iliruhusu mazungumzo ya kuanzisha serikali sambamba kuendelea licha ya kuhakikisha vinginevyo. Hayo yanajiri baada ya Rais Ruto kuruhusu wanamgambo wa Sudan waliowekewa vikwazo kufanya mkutano jijini Nairobi ili kuzindua serikali mjini Khartoum.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amefikishwa katika mahakamani ya kiraia kwa muda mfupi wakati ambapo mawakili wake walijaribu kutafuta kuachiliwa kwake, hata hivyo hakimu amesema yupo katika hali mbaya. Kuendelea kuzuiliwa kwa kunavutia maoni zaidi huku wafuasi wake , wanaharakati pamoja na watu wengine wakionya kwamba anahitaji huduma ya matibabu na anapaswa kutolewa kutoka gerezani.