Taarifa ya Habari 22 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema kampeni ya La kwa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni, inajaribu kupotosha watu dhidi yakuwatambua wa Australia wa kwanza nakuanzisha tume ya ushauri katika katiba.


Kiongozi wa zamani wa NSW Nick Greiner ame hamasisha chama cha Liberals, kiunge mkono mapokezi mapana zaidi yakibinadam, na chama hicho kibadili msimamo wacho kwa waomba hifadhi.

Mamia yamaelfu ya watu wanaweza pokea marejesho ya kodi yaliyo punguzwa mwaka huu, baada ya ofisi ya kodi ya Australia, kufufua kimya kimya madeni ya takriban watu laki tatu. Madeni hayo yakihistoria yalikuwa yame sitishwa kwa muda wakati wa moto wa vichaka wa majira ya joto yaliyo pewa jina la Black Summer Bushfires mnamo mwaka wa 2020 na katika janga la UVIKO, ila ATO sasa ime amua kurejesha dola milioni 274 ambazo inawadai.

Hakimu mkuu wa mahakama ya familia amesema unyanyasaji wakifamilia ni aibu ya kitaifa. Hakimu Will Alstergren amesema data ya mahakama inaonesha unyanyasaji wa familia, ume dai 83% ya kesi za wazazi katika mwaka wa fedha ulio pita. Mahakama inatoa filamu tatu fupi zenye lengo laku kabili mada za unyanyasaji katika kesi za sheria za famliia, umuhimu wakusikiza sauti zawatoto pamoja na jinsi mchakato wa sheria unavyo tumika.

Jumuiya kuu ya kanda ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imekataa pendekezo la utawala wa kijeshi wa Niger la kufanya uchaguzi ndani ya miaka mitatu, na kuzidisha mzozo wa kisiasa ambao unaweza kusababisha uingiliaji wa kijeshi, iwapo hakuna makubaliano yataafikiwa kufuatia mapinduzi ya mwezi Julai.

Watu sita wameuawa, wakiwemo wanajeshi wawili, Jumatatu, Agosti 21, baada ya watu wasiojulikana waliokuwa na silaha kushambulia ngome ya wanajeshi wa FARDC huko Musekere, eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri.

Rais wa zamani Donald Trump anasema atajisalimisha kwa mamlaka katika jimbo la Georgia siku ya Alhamisi kujibu mashtaka katika kesi inayomtuhumu kwa kupanga njama kinyume cha sheria, ya kugeuza matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 katika jimbo hilo.

Share