Wa Australia watapata huduma za ziada takriban milioni 18 kutoka kwa madaktari kila mwaka, kama sehemu ya ahadi kubwa ya kampeni ya uchaguzi mkuu kutoka serikali ya shirikisho.
Wamiliki wa App yamawasiliano ya Telegram wame pewa faini ya takriban $1 milioni na msimamizi wa usalama wa mtandaoni wa Australia, kwa kufeli kujibu tarehe ya mwisho ya ripoti ya uwazi. Julie Inman Grant ni Kamishna wa eSafety, amesema kuchelewa huko kume zuia uwezo wa msimamizi kufanya kazi yake chini ya sheria ya Usalama wa Mtandaoni kwa takriban nusu ya mwaka. Ame ongezea kuwa moto huo unatuma ujumbe mhimu kwa sekta kuhusu kuwa na uwazi kwa muda pamoja na kufuata sheria za Australia.
Wakaaji wa Queensland wana onywa wajiandae kukabiliana na kimbunga, pamoja na wiki nzima ya hali mbaya ya hewa. Kimbunga Alfred, kume undwa kilomita 840 kutoka pwani ya kaskazini mashariki ya Queensland nakupewa kiwango cha 1 katika tukio siku ya Jumapili 23 Februari, na kime tabiriwa kuelekea katika ukanda wa kusini mashariki katika siku saba zijazo. Angus Hines ni afisa wa ngazi ya juu katika shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa, amesema imetabiriwa kuwa kiwango cha pili cha kimbunga chaki tropiki na, kinatarajiwa kuathiri mazingira ya hewa kwa wakaaji wa pwani.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Jumapili alisema uongozi mbaya wa mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi umechangia pakubwa kwa kuzidisha mzozo mashariki mwa nchi. Mzozo huo sio tu kutokana na kusonga mbele kwa kundi la waasi la M23 ambalo inasemekana linaungwa mkono na Rwanda au mvutano kati ya Kinshasa na Kigali, Kabila aliandika katika makala ya maoni kwenye gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times.
Vikosi vya akiba vya Sudan (RSF) na washirika wake Jumapili wamekubaliana kuunda serikali ya pamoja, licha ya onyo kwamba hatua hiyo inaweza kuisambaratisha zaidi nchi hiyo iliyoharibiwa na vita. Pande za makubaliano hayo, zilitia saini katika mkutano wa faragha Nairobi, Kenya, na kusema mkataba huo unaanzisha serikali ya amani na umoja katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika.