Shirika la Reconciliation Victoria lime kosoa kinacho dai kuwa ni majaribio yaku punguza haki za watu wa Mataifa ya Kwanza. Hali hiyo imejiri katika jibu kwa kauli ya kiongozi wa upinzani Peter Dutton, kuwa hata zungumza mbele ya bendera zawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait kama atakuwa Waziri Mkuu. Baadhi ya halmashauri za jiji kote nchini Australia, yanafuta sherehe zaukaribisho nchini.
Uganda imeongeza kiwango cha tahadhari kutokana na mlipuko wa homa ya Marburg nchini Tanzania. Nchi hiyo ya Afrika Mashariki imeongeza kiwango chake cha tahadhari kufuatia taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu mlipuko unaoshukiwa kuwa wa homa ya Marburg katika nchi jirani ya Tanzania na kusababisha vifo vya watu tisa.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimetua kiongozi wake mpya kuelekea uchaguzi Mkuu wa urais wa mwezi Oktoba. Freeman Mbowe, ambaye amekuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi cha miongo miwili, kupitia mtandao wake wa X zamani ukiitwa Twitter amempongeza mrithi wake na mkamu wake wa zamani Tundu Lissu kwa uteuzi wake. Uteuzi wa Lissu unakuja wakati huu ambapo tofauti zikionekana kuibuka ndani ya chama hicho cha upizani, changamoto ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda ikikadhoofisha chama kuelekea uchaguzi Mkuu.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.