Taarifa ya Habari 26 Juni 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Wabunge huru wamkosoa vikali Waziri Mkuu, baada yakupunguziwa idadi yawafanyakazi.


Mfuko wa mshahara wa kila mwaka kwa kiongozi wa jimbo la Victoria Daniel Andrews, utakaribia nusu milioni ya dola, kama sehemu ya ongezeko ya mshahara wa wabunge wa jimbo hilo. Kiwango cha chini cha kila mwaka pamoja na nyongeza ya mishahara ya wabunge wa Victoria, pamoja na posho zao za gharama, zitaongezeka kwa 2.75% kuanzia Julai mosi baada ya uamuzi ulio tolewa na mahakama huru ya mishahara ya Victoria.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema zaidi ya watoto 800 wamepoteza mawasiliano na familia zao kufuatia mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Afisa mawasiliano wa shirika hilo, Irene Nakasiita amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema kwamba watoto 716 wameorodheshwa nchini Uganda pekee, huku wengine155 wakiwa wameunganishwa na familia zao.

Polisi nchini Uingereza wamewafungulia mashtaka mwanasiasa mmoja wa Nigeria,pamoja na mkewe , kwa kupanga njama za kumpeleka mtoto mwenye umri wa miaka 15 hadi Uingereza ili kumtoa sehemu za viungo vya mwili.


Share