Taarifa ya habari 27 Disemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Mabadiliko mazuri ya hali ya hewa yame saidia juhudi za wazima moto wanao kabiliana na moto ambao haukuwa ukidhibitika katika maeneo ya Grampians jimboni Victoria, baada ya hali mbaya zaidi ya hali ya hewa kwa moto wa vichaka tangu tukio la Black Summer la 2019.


Matokeo ya kura ya maoni ya kampuni ya Newspoll yamedokeza kuwa jimbo la Victoria lita jiunga na jimbo la New South Wales kama maeneo muhimu yakuwaniwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakati jeshi la DRC, likiendelea na operesheni dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo waasi wa M23 wanao ripotiwa kusaidiwa na Rwanda, ripoti zinaonesha rais Felix Tshisekedi anaendelea kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kuendana na wakati. Katika mabadiliko hayo, Luteni Jenerali Pacifique Masunzu anachukua nafasi ya kamanda katika maeneo ya Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini, maeneo yaliyokosa utulivu.

Jeshi la polisi Kenya limekanusha kuhusika na visa vya karibuni vya utekaji unaowalenga wakosoaji wa serikali. Watu 74 walitekwa tangu maandamano ya kuipinga serikali, huku 26 wakiwa bado hawajulikani waliko.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share