Taarifa ya Habari 27 Julai 21

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Jimbo la New South Wales limerekodi vifo 10 vinavyotokana na virusi vya corona kupitia mlipuko wa hivi karibuni wa gonjwa hilo.


Waziri wa Afya wa New South Wales amesema, anatarajia kuna uwezekano wa vifo vingi vya virusi vya corona ikiwa idadi ya kesi katika jimbo ikiongezeka.

Katika habari za Kimataifa:

Takriban watu 57 wamekufa maji baada ya mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji kupinduka katika pwani ya Libya.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji [[IOM]] linasema wanawake wasiopungua 20 na watoto wawili walikuwa miongoni mwa wale waliozama.
 
Na huko India, takriban watu saba, wakiwemo maafisa sita wa polisi, wameuawa na zaidi ya 70 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya majimbo mawili nchini humo. 
 

Share