Mwanasheria mkuu wa New South Wales amesema jeshi la polisi halina uhakika kilicho fanywa na faili elfu 9 zilizo pakuliwa kutoka tovuti ya serikali katika tukio kubwa la kuvujwa kwa data. Taarifa ya polisi imesema faili hizo zilichukuliwa kutoka Idara ya Jumuiya na Haki, zinajumuisha amri zakusitisha vurugu na hati za kiapo, ambazo wataalam wa sheria wana hofu inaweza waweka waathiriwa wa unyanyasaji wa nyumbani hatarini.
Utawala wa Trump umejaribu kudhibiti utata ulio ibuka kutoka kwa taarifa zilizo vuja kuwa mwandishi wa habari, ali ongezwa katika kundi la mazungumzo ya viongozi wa ngazi ya juu ya serikali katika mtandao wa mawasiliano wa Signal, ambako maswala kuhusu mipango ya mashambulizi dhidi ya wapiganaji waki Houthi yali changiwa. Jarida la The Atlantic lime chapisha baadhi ya mawasiliano yaliyo changiwa katika mtandao wa Signal baada ya taarifa kuvuja kuwa mhariri wa jarida hilo alikuwa ame ongezwa katika kundi hilo.
Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Salva Kiir, amekamatwa jana Jumatano, hatua iliyoelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa inaiweka nchi hiyo katika ukingo wa mzozo mpana zaidi.