Taarifa ya Habari 28 Agosti 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Swala la afya laendelea kuwa hoja mhimu katika kampeni za uchaguzi wa Victoria, serikali ya jimbo hilo kulipa karo ya wanafunzi wa uuguzi.


Serikali ya New South Wales imetetea gharama ya mwisho, ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa Allianz katika sherehe ya kufungua uwanja huo mjini Sydney mapema hii leo. Kiongozi wa jimbo hilo Dominic Perrottet amesema bei ya mwisho ya $828 milioni, daima ilikuwa kadirio. Aliwaeleza wandishi wa habari kuwa uwekezaji huo ulikuwa mhimu kwa mafanikio na burudani ya wakaaji wa jimbo hilo.


Wakimbizi wanao hitaji msaada wa haraka wa uhamisho, wame tua nchini Australia chini ya mradi mpya wa majaribio. Mpango mpya wa majaribio ya jumuiya yawakimbizi na majiribio ya makazi, unaruhusu vikundi vya jamii kote nchini Australia, kusaidia familia kupata makaazi, mwelekeo wa ndani, elimu na huduma za serikali. Ukiungwa mkono na serikali ya shirikisho, mradi ambao umepewa jina la ufipi la CRISP, unatumai kutoa mapokezi kwa wakimbizi wapya elfu moja miatano katika muda wa miaka mitatu ijayo.


Ushahidi kutoka kwa mwanaharakati anayepambana na ufisadi nchini Kenya, John Githongo, kuunga mkono madai ya mgombea urais Raila Odinga, kwamba mfumo wa matokeo ya uchaguzi ulidukuliwa ili kumpokonya ushindi unashabihiana na waraka uliowasilishwa mwaka wa 2017. Miaka mitano iliyopita, Bw Odinga pia alipinga matokeo ya uchaguzi na Mahakama ya Juu ikaamuru urudiwe.

Share