Alipo zungumzia swala shtuma hilo, Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema serikali ilikuwa na taarifa kuhusu uwepo wa meli za China, na jeshi za Australia pamoja na New Zealand zilikuwa ziki fuatilia kundi hilo.
Jeshi la polisi lina omba umma kuepuka sehemu za fukwe kuu ya Gold Coast baada ya kifaa kilicho tiliwa shaka kusukumwa na maji katika fukwe hiyo. Polisi wako katika fukwe ya Main Beach, baada ya waokoaji wa maisha pamoja na mtu aliyekuwa akitembea na mbwa wake fukweni kugundua kifaa hicho mida ya saa kumi na mbili na kasorobo ya Alhamisi.
Kiongozi wa jimbo la Victoria Jacinta Allan ametangaza kuwa awamu inayo fuata ya serikali ya jimbo kwa mradi wayo wakujenga vituo vingi zaidi vya shughuli, kama sehemu ya mpango wayo wakuongeza idadi ya nyumba jimboni kote. Tangazo hili linajiri wakati jimbo la Victoria siku chache zilizo pita, alisasisha sheria zao za upangaji wa maeneo ya makazi, kupiga jeki utoaji wa nyumba, nakuruhusu utaoji wa vibali kwa kasi pamoja na uhakika zaidi kwa nyumba za chini na zenye gorofa tatu.
Mamlaka ya Vatican imechangia taarifa mpya kuhusu afya ya Papa Francis. Papa ameonesha “uboreshaji kidogo” anapo endelea kukabiliana na ugonjwa wa nimonia ndani ya hospitali ya Gemelli mjini Rome, ambako amekuwa akilazwa kwa siku 13 sasa.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Jumatano alisema mahakama za kimataifa zimeshindwa kukomesha ukatili wa miongo mitatu katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Eneo la mashariki mwa DRC, ambalo limekumbwa na miongo kadhaa ya mzozo usiokoma, limetumbukia katika machafuko mapya baada ya waasi wa M23 kuteka maeneo makubwa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Nchini Sudani Kusini, hali ya wasiwasi inaongezeka tena licha ya wito wa kuheshimiwa kwa makubaliano ya amani. Chini ya mkataba huu uliotiwa saini mwaka wa 2018, serikali ya umoja wa kitaifa na mpito iko mjini Juba. Rais Salva Kiir na mpinzani wake wa kihistoria, Makamu wa Rais Riek Machar, kwa hivyo wanagawana madaraka. Lakini tangu mwanzoni mwa mwaka, makabiliano ya moja kwa moja kati ya vikosi vyao vya kijeshi yameripotiwa katika mikoa kadhaa. Jumanne Februari 25, upinzani ulishutumu kulipuliwa kwa kambi yake moja ya kijeshi na jeshi la Sudani Kusini kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.