Taarifa ya Habari 28 Februari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Wanasiasa wakuu wa Australia wamesema hatma ya mkataba wenye thamana yama bilioni ya dola na Marekani ume hakikishwa, baada ya Rais Donald Trump kuonekana nikama amesahau jina la mkataba huo wa nchi tatu zinazo jumuisha Uingereza.


Kesi mbili mpya za surua zimegunduliwa mjini Melbourne, mamlaka wa afya wa Victoria wakitoa onyo kuhusu virusi hivyo. Ugonjwa huo wenye uambukizi mkubwa kupitia hewa, unaweza sababisha wasiwasi mkubwa waki afya unao jumuisha nimonia na, encephalitis, ila katika kesi nyingi italeta dalili zinazo jumuisha upele, homa, kutokwa makamasi pamoja na kukohoa.

Takriban ujenzi wa nyumba mpya 9,000 umeharakishwa kupitia mchakato wa utoaji wa vibali jimboni New South Wales, kushughulikia ukosefu wa utoaji wa makazi. Wakipata idhini ya mwisho, makazi yatajengwa katika miradi 18, 17 kati yazo itakuwa Sydney na mradi mmoja utakuwa katika kanda ya New South Wales.

Hospitali za kibinafsi,Kenya zagomea mpango wa serikali wa bima ya afya,zikituhumu serikali kushindwa kulipa deni kubwa. Huduma za afya katika hospitali za kibinafsi zimeendelea kauthirika kwa siku ya pili sasa baada ya hospitali zaidi binafsi kujiunga kwenye mgomo wa kupinga mpango wa bima ya afya ya serikali. Hii ni baada ya muungano mwingine mwa hospitali za kibinafsi,kutangaza kusitisha utoaji huduma kwa wagonjwa wanaotumia bima ya SHA kwa msingi serikali imeshindwa kulipa deni inazodai hospitali hizo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amefanya ziara ya saa kadhaa mjini Mogadishu siku ya Alhamisi, kwa lengo la kuimarisha makubaliano dhaifu ya maridhiano kati ya nchi hizo mbili kufuatia ugomvi juu ya ushirikiano wake na jimbo lililojitenga la Somaliland. Bw Abiy alipokelewa na Rais Hassan Sheikh Mohamud na kuwa na mazungumzo yaliyohusu masuala ya amani na usalama, uchumi, diplomasia na uwezekano wa kushirikiana katika miradi ya pamoja na miundo mbinu. Mivutano kati ya nchi hizo mbili ilizuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya Ethiopia kufikia makubaliano na jimbo lililojitenga la Somaliland ili kupata njia ya kufika baharini.

Watu kadhaa wanahofiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili na ufyetuaji risasi huko Kongo. Haya yamefanyika kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na kiongozi wa kundi la AFC linalowajumuisha waasi wa M23, Corneille Nangaa, kwenye mji wa Bukavu, mashariki mwa Jmahuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mikanda ya video na picha za mnato zilizosambaa mitandaoni zinaonesha umati wa watu ukikimbia kutoka eneo la mkutano huku chini kukiwa na miili ya watu iliyojaa damu. Milipuko na milio ya risasi ilitokea wakati viongozi wa kundi la M23 wakiongozwa na Nangaa wakitoa hotuba mbele ya mamia ya wananchi waliodhuria mkutano huo.

Share