Serikali ya Shirikisho na Serikali ya Magharibi Australia zita tumia $700 milioni, kupanua barabara kuu katika mji wa Perth. Kiongozi wa upinzani Peter Dutton, ambaye pia yuko Magharibi Australia, ali ahidi kutoa kiwango sawia na kile ambacho serikali ime ahidi.
Moto wa vichaka unao waka bila kudhibitika umesababisha amri za kuhama kwa miji kadhaa katika eneo la Magharibi Victoria usiku wa jumatatu. Wakaaji wa miji ya Dimboola, Pimpinio, na Wail wali ambiwa watafute makazi wakati moto huo unaendelea kuchoma sehemu kubwa ya mbuga ya Little Desert National Park.
Milipuko ya mizinga imeitikisa Goma Jumatatu, saa chache baada ya wanajeshi wa Rwanda na wapiganaji kundi la waasi la M23 kuingia mjini humo. Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu mgogoro unaokaribia kutokea. Mpaka kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) karibu na mji wa Goma uliojaa majeshiumefungwa Jumatatu, chanzo kutoka ubalozi wa Ulaya na mashahidi walisema, saa chache baada ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda kuingia mji huo mkuu wa mkoa wa Kongo Mashariki. Rwanda imekana kuhusika licha ya ripoti za kuaminika kutoka Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwa inawaunga mkono waasi wa M23.
Kupitia gazeti rasmi la serikali, rais wa Kenya, William Ruto, ameteua jopo ambalo litaendesha shughuli nzima ya kuwateua makamishna wa tume ya Uchaguzi IEBC, hii ikiwa ni hatua muhimu ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.