Wa australia hawata pewa afueni ya ziada ya ushuru chini ya serikali ya mseto, badala yake kiongozi wa upinzani Peter Dutton amependekeza utoaji wa umeme na mafuta ya bei nafuu.
Mkuu wa jeshi la Sudani Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema Jumatano jioni kwamba Khartoum "imekombolewa," baada ya hapo awali kutangaza kwamba vikosi vyake vimeutwaa tena uwanja wa ndege wa mji mkuu, eneo la kimkakati na la kishara lililokaliwa tangu kuanza kwa vita na na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kwa jina la Hemedti.
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya SADC, wameongeza kasi ya kujaribu kusuluhisha mzozo wa mashariki mwa nchi ya DRC, ambapo wametangaza kuongeza timu ya wapatanishi kufuatia kikao chao cha Jumatatu ya wiki hii.