Taarifa ya Habari 28 Novemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Upinzani wa shirikisho unaendelea kuikosoa serikali baada ya hukumu ya mahakama kuu, kuamuru kuwa kuweka watu ndani ya vizuizi vya uhamiaji kwa muda usiojulikana nchini Australia ni kinyume cha sheria.


Serikali ya Alabanese imetoa mwongozo wa uchunguzi kwa tukio la kupotea kwa huduma za Optus nchini kote mwezi huu. Taarifa kutoka Waziri wa Mawasiliano Michelle Rowland, imesema uchunguzi huo uta ongozwa na naibu mwenyekiti wa zamani wa mamlaka ya mawasiliano na vyombo vya habari vya Australia Richard Bean. Jukumu la uchunguzi huo niku fanya tathmini ya kile ambacho serikali, sekta na jamii inaweza jifunza kupitia ukosefu wa huduma hiyo.

Waandalizi wa maandamano ya manzingira katika mji wa Newcastle jimboni NSW Jumapili, wamesema hawana majuto yoyote kuhusu matendo yao, licha ya idadi ya watu 100 kufunguliwa mashtaka yanayo husiana na maandamano hayo. Watoto watano ni miongoni mwa watu walio kamatwa pamoja na mwanaume mwenye miaka 97, ambaye ni mmoja wa watu wenye umri mkubwa zaidi kufunguliwa mashtaka nchini Australia.

Serikali ya shirikisho itawasilisha muswada wiki hii, waku dhibiti malipo ya huduma zakidijitali. Muswada huo utasaidia Benki kuu kudhibiti mifumo kama Apple Pay, Google Pay, na huduma zingine kama hizo, vile inavyo dhibiti kadi za mikopo pamoja na huduma za EFTPOS.

Qatar imetangaza hivi punde kwamba makubaliano yamefikiwa ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano ya kibinadamu kwa siku mbili zaidi. Makubaliano hayo yalitarajiwa kumalizika baada ya leo. Qatar imekuwa ikipatanisha mazungumzo kati ya Israel na Hamas.


Jeshi la polisi nchini Tanzania limemhoji aliekuwa naibu waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekuli kwa tuhuma za kumfanyia ukatili mfanyakazi ambaye amedai aliingizwa chupa kwenye sehemu za siri akidaiwa kutaka kumuua. Wakati polisi ikimhoji Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul kufuatia tuhuma za ukatili na unyanyasaji dhidi ya mfanyakazi wake Hashim Ally, wanasheria na wanaharakati wa haki za binadamu wametoka hadharani na kutaka hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya mbunge huyo endapo tuhuma zinazomkabili zitathibitika kuwa za kweli.

Baraza la Magavana Nchini Kenya linataka Baraza la Kitaifa la Mtihani, lisuluhishe utata ambao ulishuhudiwa kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la nane 2023 ambapo kulikuwa na mchanganyiko wa alama. Baadhi ya wanafunzi walipata matokeo kwenye masomo ambayo hayakuwa yao huku masomo ya Kiingereza na Kiswahili yakiathirika pakubwa.




Share