Mfuko wa mswada wa uhamiaji wa serikali ya Labor, ulipitishwa ndani ya seneti jana usiku wa Alhamisi 28 pakiwa mjadala mdogo, na upinzani wa mseto uliunga mkono muswada huo.
Kamishna wa kitaifa wa watoto, Anne Hollonds, amesema marufuku ya mtandao wakijamii kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka 16 haitafanya mitandao hiyo kuwa salama zaidi. Marufuku ya serikali yalipitishwa ndani ya Seneti na yata anza kutumiwa mwisho wa mwaka ujao, kuzipa kampuni za mitandao yakijamii muda waku tii au kukabiliwa na faini ya hadi milioni $50.
Serikali ime wa onya wa Australia wawe tayari kwa vimbunga, mafuriko na mawimbi ya joto kali katika msimu wa majira ya joto, wakati sehemu nyingi za Australia zina tarajiwa kukabiliana na hatari kubwa ya moto wa vichaka. Baraza la mamlaka ya huduma ya dharura na moto ya Australasia, sasa imetoa mtazamo wayo wa msimu wa joto wa 2024, unao onesha sehemu nyingi za Kusini Australia na vijiji vyakikanda katika Wilaya ya Kaskazini zina hitaji jitayarisha. Ramani ya mtazamo pia ina onesha vitisho vilivyo ongezeka katika pwani ya kusini ya Magharibi Australia na takriban nusu ya Victoria.
Wanunuzi wa Australia wana tarajiwa kutumia zaidi ya $6 bilioni [[$6.7]] wakati wa mauzo ya Black Friday na Cyber Monday. Utafiti wa Roy Morgan umepata matumizi yata ongezeka mwaka huu, watu wanapo tafuta bidhaa za punguzo za bei wakati huu wa janga la gharama ya maisha. Mauzo ya Black Friday sasa, yamepita mauzo ya Boxing Day kama tukio la mauzo maarufu nchini.
Takribani watu 30 wanahofiwa kufa baada ya kutokea maporomoko ya ardhi katika kijiji kimoja mashariki mwa Uganda. Hayo yamesemwa na afisa mmoja wa eneo hilo aliyeonya kuwa idadi hiyo huenda ikapanda. Mkuu wa Wilaya ya Bulambuli, Faheera Mpalanyi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa maporomoko ya ardhi yalitokea katika kijiji cha Masugu na kuwa miili sita, ukiwemo wa mtoto mdogo, imepatikana mpaka sasa.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), karibu robo ya wakazi, au zaidi ya watu milioni 25, wanakabiliwa na njaa, ikiwa ni pamoja na milioni tatu wakiwa katika ali ya dharura za kibinadamu. Ili kukabiliana na mgogoro huu, FAO (Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa) linakadiria kuwa linahitaji dola milioni 330.
Mtanzania Faustine Ndugulile, ambaye angeingia madarakani kama mkurugenzi wa kikanda wa Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Afrika mwezi Februari, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55, Rais wa Bunge la Tanzania ametangaza siku ya Jumatano.